Blogger Tips And Tricks|Latest Tips For BloggersFree BacklinksBlogger Tips And Tricks

Tuesday, February 10, 2015

Moto mkubwa umeteketeza ghorofa ya pili ya jengo la Consolidated Investment Tanzania Limited jijini Dar es Salaam.

Moto mkubwa umeteketeza ghorofa ya pili ya jengo la Consolidated Investment Tanzania Limited jijini Dar es Salaam.
Moto mkubwa umeteketeza kabisa ghorofa ya pili ya jengo la Consolidated Investment Tanzania Limited huku baadhi ya familia zinazoishi katika ghorofa ya kwanza ya jengo hilo wakiwemo watoto wakinusurika baada ya kuokokolewa na jeshi la polisi jijini Dar es Salaam.
Moto huo mkubwa ambao chanzo chake hakikufahamika mara moja umeteketeza kabisa ghorofa ya pili ya jengo hilo la Consolidated Investment Tanzania Limited lililopo katika mtaa wa Libya na msikiti Kisutu jijini Dar es Salaam huku mashuhuda wa moto huo wakionekana wakiwa makini kupiga picha katika simu zao pengine kutokana na kukuwa kwa teknolojia.
 
Jeshi la polisi lilifika mapema katika eneo la tukio wakiongozwa na kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova kwa nia ya kuimarisha ulinzi na kuzuia tabia iliyozoeleka ya baadhi ya wakazi wa jiji kutumia majanga ya moto na ajali kama fursa ya kujipatia chochote ambapo mashuhuda wamelizungumzia tukio hilo.
 
Akizungumza mara baada ya moto huo kuzima kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam amewaambia waandishi wa habari kuwa upelelezi wa kitaalam, juu ya chanzo cha moto huo bado unaendelea na kuongeza kuwa kwa kiasi kikubwa jeshi hilo limefanikiwa kudhibiti vitendo vya kihalifu kufanyika katika tukio hilo pamoja na kufanya uokozi.
 
Jicho la tatu la ITV likashuhudia namna zimamoto walivyokuwa wakihaha kupata maji ya kutosha ya kuuzima moto huo kabla ya kuongezewa nguvu na vikosi vya zimamoto na uokoaji kutoka bandari na uwanja wa ndege wakati katika majengo jirani kukiwa na matanki lukuki yenye maji yaliyokuwa yakimwagika bila ya matumizi jambo lililochangia kwa kiasi kikubwa jengo hilo kuendelea kuteketea licha ya uwepo wa maji hayo karibu kabisa ambayo endapo yangetumika huenda madhara katika ghoro hiyo ya pili yasingekuwa makubwa kiasi hiki jambo ambalo kamishna wa kikosi cha ukoaji na zimamoto analizungumzia.